Watu 6 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa kuwa 554.
Katibu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amesema kuwa idadi ya waliopona imefika 18,895 baada ya watu 225 zaidi kupona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Idadi ya visa vya ugonjwa huo nchini imeongezeka na kufikia 32,557 baada ya visa vipya 193 kudhibitishwa.
Msambao wa visa hivyo ni kama ifwatavyo; Nairobi 78, Embu 24, Garissa 21, Kiambu 18, Nyeri 13, Murang’a 5, Kajiado 3 Machakos, Isiolo na Nakuru 1.









