Washukiwa kwenye mauji Kilimani kulala ndani

0

Washukiwa wawili waliokamatwa kuhusiana na mauji ya Kelvin Omwenga, 28 Kilimani, Nairobi watalala kizimbani wakisubiri mahakama kuamua kuhusu iwapo wataendelea kuzuiliwa Jumanne.

Wawili hao Robert Ouko na Chris Obure walifikishwa katika mahakama ya Kibera Jumatatu ambapo upande wa mashtaka umeomba wazuiliwe kwa siku kumi na nne zaidi ili kutoa nafasi ya kukamilika kwa uchunguzi.

Ouko aliifahamisha mahakama kwamba risasi iliyomuua Omwenga ilifyatuka kimakosa wakati walikuwa wanapigania bastola.

Polisi aidha wanachunguza sakata ya dhahabu ambayo inahusishwa na tukio hilo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here