Aliyekuwa mbunge Masoud Mwahima aaga dunia

0

Aliyekuwa mbunge wa Likoni Masoud Mwahima ameaga dunia nyumbani kwake Vyemani kaunti Mombasa.

Familia yake inasema mwendazake alifariki mwendo wa saa tano jana usiku baada ya kuugua pumu (asthma) ugonjwa ambao husababisha mtu kubanwa mbavu na kushindwa kupumua.

Msemaji wa familia amewaambia wanahabari kuwa mwendazake alikuwa hospitalini siku ya Jumapili kupokea matibabu na kuwa amekuwa akiugua kwa muda mrefu.

Mwahima mwenye umri wa miaka 78 alipoteza kiti hicho cha Likoni kwa mbunge wa sasa Mishi Mboko kwenye uchaguzi mkuu uliopita.

Amekuwa mbunge wa eneo hilo kuanzia mwaka 2007 kwa tiketi ya chama hicho cha ODM ambacho alitumia kutetea kiti chake mwaka elfu mbili na kumi na tatu.

Hata hivyo alikigura chama hicho na kujiunga na Jubilee mwaka 2016 kabla ya kubwagwa na Mihsi Mboko katika uchaguzi uliofuatia mwaka 2017.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here