Watu 14 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa wa corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 884.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amearifu kuwa watu wengine 631 wameambukizwa virusi hivyo baada ya kupima sampuli 6,142 na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 47,843.
Wagonjwa walio katika chumba cha watu mahututi ni 20 huku 59 wakisaidiwa na mashine kupumua.
Idadi ya waliopona ugonjwa huo imeongezeka na kufika 33,421 baada ya watu 371 kupona.
Nairobi inaongoza na visa 235, Mombasa 76, Kilifi 52, Kisumu 30, Uasin Gishu 28, Bungoma & Busia 23, Kiambu 22, Machakos 21, Nyeri 15, Kajiado 13, Homabay & Kisii 12,Trans Nzoia 11, Meru 10, Siaya 7, Turkana 6, Elgeiyo Marakwet 6, Kakamega 4, Marsabit, Nakuru, Narok, Embu 3, Nyamira Nandi, Makueni & Vihiga 2,Nyandarua ,TharakaNithi, Muranga, Isiolo na Kwale 1.









