Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa ameachiliwa kwa dhamana ya Sh4M huku mlinzi wake Geoffrey Okuto akiachiliwa kwa dhamana ya Sh1.5M pesa taslimu baada ya kukanusha mashtaka ya kumuua Ngumbao Jola.
Wawili hao wameachiliwa kwa dhamana na jaji Njoki Mwangi baada ya kulala seli kwa muda wa siku nne wakisubiri hatma yao.
Jaji huyo aidha amemuagiza Jumwa na mshtakiwa mwenza kuwasilisha pasipoti zao mahakamani.
Wawili hao wamekanywa dhidi ya kusafiri pasipo kutoa sababu za kutosha na kuhitilafiana na mashahidi kwenye kesi hiyo.
Jumwa na Okuta walikanusha mashtaka ya kumuua Jola mwenye umri wa miaka 48 mkesha wa uchaguzi mdogo wa Ganda, kaunti ya Kilifi Octoba 15 mwaka jana.