Gavana Sonko apata afueni

0

Mahakama ya Leba imeongeza muda wa maagizo yanayolizuia bunge la kaunti ya Nairobi kujadili hoja ya kumwondoa gavana Mike Mbuvi Sonko.

Jaji Byrum Ongaya ameagiza uamuzi huo kuzingatiwa hadi kesi hiyo itakaposikilizwa huku akipuuzilia mbali ombi la spika wa bunge hilo aliyehoji kuwa mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi hiyo.

Jaji huo ameamuru kuwa mahakama hiyo ina uwezo wa kuingilia kati na kusikiliza kesi inayohusiana na ukiukaji wa haki za mfanyikazi yeyote.

Kesi hiyo inatarajiwa kutajwa tena Octoba 27.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here