Linda Katiba wapiga marekebisho ya katiba

0

Vuguvugu la Linda Katiba limewataka Wakenya kukataa marekebisho ya katiba kupitia mchakato wa BBI.

Kundi hilo likiongozwa na kiongozi wa chama cha NARC-K Martha Karua limefananisha marekebisho hayo na mapinduzi ya katiba ya mwaka 2010.

Linda Katiba wanasisitiza kwamba rais Uhuru Kenyatta na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga wanapanga kutumia marekebisho ya BBI kugawana mamlaka baada ya uchaguzi mkuu wa 2022.

Wanahoji kwamba mabadiliko hayo ya kisheria yatawapkonya Wakenya nafasi ya kuwachagua viongozi wao na kuwapa watu wachache wenye ushawishi fursa ya kumchagua wanayetaka kuwa rais.  

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here