Kanisa katoliki lajitenga na msimamo kwamba chanjo ya corona sio salama

0

Kanisa katoliki nchini limejitenga na msimamo kwamba chanjo dhidi ya ugonjwa wa corona inayoendelea kutolewa nchini sii salama.

Muungano wa maaskofu wa kanisa hilo (KCCB) kupitia mwenyekiti Philip Anyolo umesema msimamo huo uliotolewa na muungano wa madaktari wa kanisa hilo (KCDA) sio msimamo halisia wa kanisa hilo na kwamba ni mtazamo wa binafsi.

Maaskofu hao vile vile wameirai wizara ya afya kuendelea kutoa chanjo hiyo kwa wale wanaotaka kupewa kwa hiari na wala sio kwa kulazimishwa.

Itakumbukwa kwamba madaktari hao wa kanisa katoliki waliwataka Wakenya kujiepusha na chanjo hiyo kwa misingi kwamba sii salama na kwamba ina madhara ya kiafya kwa watakopewa.

Hayo yakijiri

Shuguli ya kutoa chanjo ya corona kwa wahudumu wa afya na  wafanyikazi wengine walio hatarini kuambukizwa virusi vya covid 19 inaendelea katika kaunti mbalimbali nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here