Bunge la kaunti ya Uasin Gishu limekuwa la kwanza kususia kujadili mswada wa marekebisho ya katiba BBI.
Madiwani wa bunge hilo wamesema hatma ya mswada huo inasalia na Wakenya watakaofanya uamuzi wa mwisho kupitia kwa kura ya maamuzi.
Madiwani wapatao 27 waliunga mkono ripoti ya kamati ya bunge hilo kuhusu sheria iliyosema kuwa wasipige kura ya NDIO au LA kwa mswada huo.
Mswada huo ulioko bungeni umepitishwa na mabunge 43 na kukataliwa na mabunge matatu pekee ambayo ni Baringo, Nandi na Elgeyo Marakwet.









