Watu 337 wameambukizwa virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 2,924 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 109,164.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa watu 53 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 87,623.
Wagonjwa 3 zaidi wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,879.
Watu 532 wamelazwa katika hospitali mbalimbali 74 wakiwa katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 40 wakisaidiwa na mashine kupumua.