Aliyekuwa waziri wa Michezo Rashid Echesa atasalia korokoroni Jumanne wakati mahakama itatoa uamuzi wa ombi la upande wa mashtaka kutaka kumzuilia zaidi.
Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Kiambu Patricia Gichuhi ameagiza Echesa kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Gigiri wakati atatoa uamuzi kuhusu ombi hilo.
INSERT: GICHUHI ON ECHESA
Afisa anayechunguza kesi hiyo ameomba mahakama kuwaruhsuu kumzuilia mwanasiasa huyo kwa muda wa siku saba zaidi ili kukamilisha uchunguzi kuhusiana na madai ya kumzaba kofi afisa wa uchaguzi na pia kuvunja sheria zingine za uchaguzi.
Hahat hivyo Echesa kupitia kwa mawakili wake wakiongozwa na Cliff Ombeta amepinga ombi hilo na badala yake kusema maafisa hao walikuwa na muda wa kufanya uchunguzi tangia siku ya Ijumaa.
Echesa alinaswa kwenye video akimzaba kofi afisa wa IEBC wakati uchaguzi mdogo wa eneobunge la Matungu siku ya Alhamisi wiki iliyopita.