Mbunge wa Kapenguria Samwel Moroto ashtakiwa kwa uharibifu wa mali

0

Mbunge wa Kapenguria Samuel Moroto ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 500,000 pesa taslimu baada ya kukanusha mashtaka ya uharibifu wa mali.

Mwanasiasa huyo amefikishwa mbele ya hakimu wa mahakama ya Kitale Symphie Makila kwa kuharibu mali yenye dhamana ya shilingi milioni 7 inayomilikiwa na shirika la maendeleo ya kilimo (CDC) mwaka 2017.

INSERT: MAKILA ON MOROTO

Mbunge huyo anashtakiwa siku moja baada ya kukamatwa na makachero wa DCI kuhusiana na utata unaozingira umiliki wa kipande cha ardhi kaunti ya Trans Nzoia.

Inadaiwa aliongza kundi la wakaazi kulisha mifugo katika eneo hilo licha ya marufuku iliyowekwa.

Kesi yake itatajwa tena tarehe 15 Machi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here