Osoro ashtakiwa kwa uchochezi, aachiliwa kwa dhamana

0

Mbunge wa Mugirango Kusini Sylvanus Osoro ameachiliwa kwa dhamana ya shilingi 100,000 baada ya kukana mashtaka ya uharibifu wa mali.

Osoro ameshtakiwa mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Kisii Nathan Shiundu kwa kosa la uchochezi na uharibifu wa gari la Peter Karanja Njuguna lenye dhamani ya shilingi 200,000 wakati wa uchaguzi mdogo wa Kiamokama.

Osoro alijisalimisha kwa maafisa wa DCI mjini Kisii ambapo alidaiwa kuchangia vurugu wakati wa uchaguzi huo wa Alhamisi iliyopita

Mbunge huyo aliwaambia wanahabari kuwa kwa maisha yake yoye hajawahi kumilki bunduki au bastola na kushutumu polisi kwa kunasa gari lake na pia kumhangaisha dereva wake na afisa wake mmoja bila sababu.

Mwakilishi wa wanawake katika kaunti ya Uasin Gishu Gladys ‘Boss’ Shollei amelalamikia kile anasema ni kuhangaishwa kwa wabunge wanaomuunga mkono naibu Rais William Ruto.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here