Kliniki ya kupima saratani yafunguliwa Laikipia

0

Kaunti ya Laikipia imekuwa ya hivi punde kupata kliniki itakayowawezesha akina mama na wasichana kupimwa ugonjwa wa saratani ya matiti.

Mkewe rais Bi. Margaret Kenyatta kupitia kwa mshirikishi wa kampeini ya Beyond Zero Angella Langat amesema lengo lake ni kuwawezesha wanawake na wasichana kupimwa saratani na kufahamu hali yao hatua itakayowawezesha kupata matibabu mapema.

Langat anasema makusudi na Bi. Kenyatta kwa ushirikiano na wake za magavana wote 47 ni kuhakikisha kuwa maafa yanayotokana na aina mbalimbali ya saratani ikiwemo saratni matiti na uzazi yamepunguzwa.

Kaunti ya Laikipia inapata kliniki hiyo baada ya Nanyuki ambayo ilipata kliniki hiyo mwezi uliopita.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here