Mvua zinazoshuhudiwa katika maeneo mbalimbali nchini zitaendelea hadi Jumanne wiki ijayo.
Idara ya utabiri wa hali ya anga inasema maeneo yakayoathirika na mvua hizi ni; Nyeri, Kiambu, Nyandarua, Laikipia, Murang’a, Embu, Meru na Kirinyaga.
Maeneo mengine yatakayoshuhudia mvua hizo ni Tharaka Nithi, Taita Taveta, Busia, Kisii, Nyamira, Kericho, Bomet, Nakuru, Baringo, Narok, Migori, Nandi, Trans Nzoia na West Pokot.
Wenyeji katika maeneo hayo wanashauriwa kutahadhari kuhusu uwezekano wa kutokea kwa mafuriko na mito kuvunja kingo zake kutokana na mvua hizo.
Wakaazi wa Uasin Gishu, Vihiga, Bungoma, Homa Bay, Busia, Kisumu, Siaya, Kakamega, Kajiado, Mombasa, Kwale, Kilifi sehemu za Tana River na Lamu vile vile zitaendelea kushuhudia mvua hizo.