Jaji mkuu David Maraga ameongoza ufunguzi wa mahakama ya hakimu katika eneo la Ol Kalou kaunti ya Nyandarua huku akisisitizia umuhimu wa idara ya mahakama kusalia huru.
Maraga ambaye ni rais wa mahakama ya upeo amesema Wakenya wanataka idara hiyo muhimu kusalia huru pasipokuwa na mwingilio wa aina yoyote ili kuwajibikia jukumu lake la kuhakikisha haki inatendekeka.
Amesema itakuwa ni kuwafeli Wakenya iwapo hawatasimama kidete kulinda uhuru huo ulioko kwenye katiba.
Kauli za Maraga zinajiri huku ripoti ya BBI ikipendekeza kubuniwa kwa tume itakayokuwa inapokea malalamishi kutoka kwa umma kuhusu utendakazi wa idara ya mahakama.









