Kipyegon, bingwa wa dunia 1500m mara ya nne.

0
Faith Kipyegon akisherehekea ushindi wake katika mashindano ya riadha duniani.

Mwanariadha Faith Kipyegon aliendeleza umahiri wake katika mbio za mita 1500 na kuipa Kenya nishani ya tatu ya dhahabu kwenye mashindano ya riadha jijini Tokyo nchini Japan baada ya kushinda katika fainali ya mbio hizo siku ya Jumanne.

Kipyegon ambaye pia ni bingwa mara tatu wa Olimpiki wa mbio hizo alimaliza wa kwanza kwa muda wa dakika 3:52.15 mbele ya mkenya mwenzake Dorcus Ewoi aliyetwaa nishani ya fedha, Muaustralia Jess Hill akiridhika na nafasi ya tatu na kutwaa shaba.

Ushindi huo ulimfanya Kipyegon kuwa bingwa mara nne wa dunia kwenye mbio hizo mfululizo kuanzia mwaka wa 2017.

Katika siku ya nne ya mashindano hayo Kenya inashikilia nafasi ya pili kwenye jedwali ikiwa na nishani tatu za dhahabu, moja ya fedha na moja ya shaba nyuma ya Marekani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here