Wiseman Were Mukhobe amefuzu kwenye hatua ya nusu fainali kwenye mbio za mita 400 kuruka viunzi kwenye mashindano ya riadha za dunia yanayoendelea nchini Japan.
Hii ni licha ya kumaliza katika nafasi ya tano kwenye kundi na kukosa katika nafasi nne za kwanza ambapo ingemwezesha kufuzu moja kwa moja.
Muda wa Were wa sekunde 48:27 uliorodheshwa nambari saba miongoni mwa wanariadha wote 24 ambao walifuzu katika kitengo hicho.
Kulikuwa na makundi matano katika kitengo hicho kila kundi likitoa wanariadha wanne wa kwanza kufuzu moja kwa moja kisha wengine wanne wenye muda bora wakijiunga nao.
Were atakuwa akitimuka nusu fainali Jumatano tarehe 17 saa tisa unusu.









