Maambukizi ya ugonjwa wa corona nchini yanazidi kupanda huku watu 829 wamepatikana na virusi hivyo kati ya sampuli 6,239 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita.
Hii kufikisha idadi ya jumla ya maambukizi nchini kuwa kuwa 111,185.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kupona kwa watu wengine 91 na kufikisha idadi hiyo kuwa 87,994.
Aidha mtu mmoja amefariki kutokana na makali ya virusi hivyo na kufikisha idadi ya maafa kuwa 1,899.
Wakati huo uo wagonjwa 566 wamelazwa katika hospitali mbalimbali nchini huku wengine 1,694 wakishughulikiwa nyumbani.









