Kenya yaandikisha maambukizi mapya 83 ya corona

0

Watu 83 zaidi wameambukizwa virusi vya corona katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita baada ya sampuli 1,732 kupimwa na kufikisha idadi ya maambukizi nchini kuwa 100,856.

Waziri wa afya Mutahi Kagwe amedhibitisha kuwa watu 29 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi ya waliopona kuwa 83,936.

Idadi ya maafa imeongezeka na kufika 1,766 baada ya watu 3 zaidi kuaga dunia.

Wagonjwa 464 wamelazwa katika hospitali mbalimbali 23 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi na 12 wakisaidiwa na mashine kupumua.

Nairobi inaongoza na visa 61, Uasin Gishu 6, Busia na Mombasa 4, Kiambu na Kilifi 2, Machakos, Migori, Kericho, Elgeyo Marakwet 1.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here