DCI yachunguza mauaji ya mwanamke Bungoma

0

Makachero wa idara ya upelelezi DCI wanachunguza mauaji ya Sarah Kimarong, mwanamke aliyepatikana ameuawa katika chumba chake cha kukodisha mjini Bungoma.

Maafisa wa usalama wanasema mauaji hayo yalibainika baada ya juhudi za nduguye kujaribu kumfikia dadake kugonga mwamba.

Taarifa ya DCI inaeleza kuwa walijibu ripoti ya nduguye na walipofika alikokuwa anaishi walipata mlango wake umefungwa kwa kufuli na walipoingia ndani walipata mwili wake ukiwa kwenye kidimbwi cha damu na kuonesha ishara za kunyongwa.

Aidha inaarifiwa kuwa marehemu alikuwa mfanyikazi anayefanya kazi kwenye afisi ya naibu kamishna wa kaunti ya Bungoma.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here