Askofu wa kanisa la AIC Dkt. Benard Nguyo afariki

0

Askofu mkuu wa kanisa la Africa Inland Church Kenya (AIC) Abraham Mulwa ametangaza kifo cha askofu Dkt. Benard Nguyo.

Dkt. Nguyo alifariki jana (Jumapili) baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Askofu Mulwa ametoa wito kwa kanisa kuendelea kuiombea familia ya marehemu wakati huu mgumu wa msiba.

Mikutano ya kupanga mazishi itaandaliwa kuanzia hapo kesho (Jumanne) katika ukumbi wa AIC Bomani saa kumi jioni.

Mazishi yanatazamiwa kuandaliwa Jumatano Februari 10 nyumbani kwake Mitaboni, kaunti ndogo ya Kathiani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here