Kaunti za Ukambani kupitisha BBI

0

Mabunge ya kaunti ya Machakos, Makueni na Kitui yameahidi kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI Jumanne asubuhi.

Haya yameafikiwa baada ya magavana Dkt. Alfred Mutua wa Machakos kukutana na mwenzake wa Makueni Profesa Kivutha Kibwana.

Dkt. Mutua na Profesa Kibwana wamesema haya baada ya kukutana na madiwani arobaini kutoka kaunti hizo ambapo kwa kauli moja wamesadiki kwamba kupitishwa kwa BBI kutawezesha kuongezwa kwa mgao wa fedha katika serikali za kaunti.

Profesa Kibwana ameonekana kulegeza msimamo kuhusu kupinga mswada huo siku chache baada ya kukutana na kinara wa ODM Raila Odinga.

Hatua hii inajiri wakati ambapo mabunge ya kaunti yamechangamkia kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI kufikia sasa kaunti 11 zikiwa tayari zimepitisha mswada huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here