Serikali yashtakiwa kuhusu mikopo ya magari kwa MCAs

0

Serikali imeshtakiwa kufuatia azimio lake la kuwapa wawakilishi wadi mikopo ya kununua magari.

Kwenye kesi yake, daktari Magare Gikenyi anahoji kuwa madiwani walijitolea kufanya kazi bila kulazimishwa na sasa si wakati wa kutaka wakenya na serikali kuingilia kati na kuwatekelezea mahitaji yao ya kibinafsi.

Magere ameitaka mahakama kusimamisha amri hiyo ambayo anahisi inakiuka sheria huku akitaka fedha hizo kutumika kwa miradi ya maana zaidi.

Haya yanajiri siku moja  baada ya mratibu wa bajeti Dkt. Margaret Nyakango kupinga hatua hiyo akisema inakiuka sheria.

Gavana wa Nakuru Lee Kinyanjui ni mongoni mwa viongozi waliounga mkono uamuzi wa kuwapa madiwani mikopo ya kununua magari.

Agizo hilo lilitolewa na rais Uhuru Kenyatta akisema pia madiwani wana haki ya kupewa mikopo ya kununua magari,wazo ambalo liliungwa mkono na kinara wa chama cha ODM Raila Odinga na tume ya kutathmini mishahara ya watumishi wa umma (SRC).

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here