Kalonzo bado anapambana na Raila

0

Kiongozi wa chama cha Wiper Kalonzo Musyoka sasa anadai kuwa mwenzake wa ODM sio mtu wa kuaminika hata na uongozi wa taifa hili.

Kwenye taarifa ya kumjibu Odinga kuhusu kutowa na deni la kisiasa, makamu huyo wa rais wa zamani ameeleza kuwa huenda Raila akakatalia afisini iwapo atachaguliwa kuwa rais.

Kalonzo ambaye wamekuwa na Odinga kwenye muungano wa upinzani NASA ametaja kuwa waziri huyo mkuu wa zamani sio mtu wa kuingia naye kwenye ushirikiano wowote wa kisiasa kwa sababu mwisho wa siku atakuacha mashakani. 

Urafiki baina ya Raila, Kalonzo, Musalia Mudavadi na Moses Wetangula umepasuka kufuatia matamshi ya Odinga kwamba hatamuunga mkono yeyote kwa sababu walimsaliti wakati wa uapisho wake pale Uhuru Park.

Mudavadi kwa upande wake amemtaja Raila kama tapeli wa siasa na mtu asiyeaminika.

Huku akisisitiza kwamba hana haja ya kuungwa mkono na kuwa hakuna aliye na deni lake, Mudavadi anasema Raila hafai kuwasuta wenzake ambao walimsaidia kujiimarisha kisiasa.

Kiongozi huyo wa chama cha Amani National Congress (ANC) anasema anajuta kutumiwa vibaya na kuhadaiwa na Raila.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here