Mratibu wa bajeti Margaret Nyakang’o sasa anasema kuwa afisi yake haipingi mpango wa kuwapa madiwani mikopo ya kununua magari.
Katika taarifa Dkt. Nyakango amesema kuwa tayari uamuzi huo umepitishwa ila kuna utaratibu mwafaka ambao unafaa kufuatwa ili kuwapa maspika na madiwani mikopo hiyo.
Akikanusha ripoti kuwa amepinga mipangilio hiyo, Dkt. Nyakango amesema afisi yake inafahamu majukumu ya kila asasi huru za kikatiba na yeye hajapinga wala kuingilia utendakazi wa asasi husika.
Maratibu wa bajeti hata hivyo amesema kinachohitajika ni kuhakikisha kwamba utaratibu wa kisheria unafuatwa ili kutowatia madiwani taabani baadaye.
Haya yanajiri siku chache baada ya tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma SRC kuidhinisha ruzuku ya shilingi billion 4.5 kwa maspika na madiwani kununua magari.