Je, MCAs walidanganywa? Serikali yajikaanga kuhusu mikopo ya magari kwa madiwani

0

Agizo la rais Uhuru Kenyatta kuwapa wawakilishi wadi ruzuku ya kununua magari imetiwa breki na mratibu wa serikali Dkt. Margaret Nyakango.

Dkt. Nyakango katika barua kwa tume ya kuratibu mishahara ya watumishi wa umma SRC amesema taratibu za kisheria zimekiukwa katika kuwapa madiwani mikopo hiyo.

Na licha ya tume ya kuratubu mishahara ya watumishi wa umma SRC kukubaliana na madiwani kupewa mikopo, mratibu wa bajeti anahoji kwamba sheria za sasa haziruhusu ruzuku ya magari kwa madiwani.

Ameongeza kuwa katika baadhi ya kaunti, maspika na madiwani wamechukua mikopo ya kununua magari na kisha kulipa pesa hizo huku wengine wakiwa bado pesa hizo hazijalipwa.

Hatua hii inajiri wakati ambapo mabunge ya kaunti yamechangamkia kupitisha mswada wa marekebisho ya katiba BBI kufikia sasa kaunti 11 zikiwa tayari zimepitisha mswada huo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here