Naibu wa Rais William Ruto na seneta wa Baringo Gedion Moi wamekutana katika mazishi ya aliyekuwa mwanasiasa Hosea Kiplagat katika kaunti ya Baringo.
Ruto ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa vijana kujiunga na taasisi za kiufundi ili kupata mafunzo yatakayowawezesha kupata ajira.
Aidha Ruto amesema kuwa serikali bado itaendelea kufanya maendeleo ya ujenzi wa barabara na kuhakikisha wakaazi hao wamepata umeme.
Kiplagat aliaga dunia tarehe 6 mwezi huu akipokea matibabu katika hospitali ya Kareni .