Idara ya Utabiri wa hali ya anga imetabiri mvua kubwa jijini Nairobi na maeneo mengine nchini wiki hii.
Katika taarifa yake ya kila wiki iliyochapishwa Machi 9, Idara hiyo imetabiri kupungua kwa jumla kwa kiwango cha mvua kote nchini kwa kipindi cha kuanzia Machi 10–16, 2026.
Hata hivyo, imeonya kwamba mvua za mara kwa mara zinatarajiwa kuendelea katika maeneo kadhaa kusini mwa Kenya.
“Mvua za mara kwa mara zitashuhudiwa katika maeneo kadhaa kusini mwa nchi,” idara imetabiri.
Matukio ya mvua kubwa bado yana uwezekano wa kutokea katika baadhi ya maeneo ya Nyanda za Juu Mashariki na Magharibi mwa Bonde la Ufa, Bonde la Ziwa Victoria, Bonde la Ufa, Nyanda za Chini Kusini-mashariki na Pwani ya Kusini.
Mawingu nyakati za asubuhi pamoja na mvua wastani inatarajiwa, kisha kutoa nafasi kwa vipindi vya jua, huku mvua za alasiri zikinyesha katika maeneo machache na mara kwa mara huenda zikaenea katika maeneo kadhaa yakiwemo Kaunti za Nyandarua, Laikipia, Nyeri, Kirinyaga, Murang’a, Kiambu, Meru, Embu, Tharaka-Nithi na Nairobi.
Kulingana na idara hiyo, mvua za asubuhi zinatarajiwa kunyesha katika maeneo chache, ikifuatiwa na mvua za alasiri na ngurumo za radi, kisha kufuatiwa na mvua za usiku.
Hii ni pamoja na kaunti za Nandi, Kakamega, Vihiga, Bungoma, Siaya, Busia, Baringo, Nakuru, Trans-Nzoia, Uasin-Gishu, Elgeyo-Marakwet, West-Pokot, Kisii, Nyamira, Kericho, Bomet, Narok, Migori, Kisumu, Nakuru na Kaunti ya Kisumu.
Katika maeneo ya Kaskazini-magharibi mwa Kenya, ikiwa ni pamoja na Kaunti za Turkana na Samburu, vipindi vya jua vinatarajiwa wakati wa mchana, hali ya mawingu kiasi usiku, huku mvua ikinyesha mara kwa mara katika maeneo chache.









