Katibu katika wizara ya afya Dkt. Mercy Mwangangi amepata chanjo ya corona katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta (KNH).
Dkt. Mwangangi amepata chanjo hiyo wakati ambapo Kenya imeripoti visa visa vipya 731 vya corona kati ya sampuli 4,513 zilizopimwa katika muda wa saa Ishirini na nne zilizopita na kufikisha idadi ya visa hivyo nchini kuwa 113,967.
Waziri wa afya Mutahi Kagwe amethibitisha kuwa wagonjwa 191 wamepona ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 88,596.
Wagonjwa 5 wameaga kutokana na ugonjwa huo kufikisha idadi ya maafa nchini kuwa 1,918.
Wagonjwa 678 wamelazwa katika hospitali mbalimbali, 109 wako katika vyumba vya wagonjwa mahututi, 23 wanasaidiwa na mashine kupumua.









