Mahakama ya Meru yafungwa, mfanyikazi akifariki kutokana na corona

0

Mahakama ya Meru imefungwa kwa siku 7 baada ya mfanyikazi mmoja kufariki kutokana na matatizo yanayoambatana na ugonjwa wa corona.

Akidhibitisha kifo hicho, naibu jaji mkuu Philomena Mwilu amesema kufungwa kwa mahakama hiyo kutawapa nafasi wafanyikazi kupimwa na kuwezesha shughuli ya kunyunyuziwa dawa.

Amesema yeyote atakayekutwa na virusi hivyo atajiweka kwenye karantini kuambatana na taratibu za wizara ya afya.

Kesi za dharura zilizokuwa zishughulikiwe katika mahakama hiyo zitahamishwa hadi katika mahakama za Githongo, Tigania na Nkubu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here