Mwili wa Jennifer Wambua wapatikana

0

Mwili wa naibu mkurugenzi wa mawasiliano katika tume ya ardhi nchini NLC Jennifer Wambua umepatikana katika hifadhi ya maiti ya City, Nairobi.

Polisi wanasema mwili wa marehemu ulipatikana katika eneo la Ngong Jumamosi.

Wambua hajaonekana kuanzia Ijumaa na ripoti ya kupotea kwake iliwasilishwa katika kituo cha Polisi cha Capitol Hill.

Mumewe Joseph Komu alikuwa amefichua kuwa alikuwa amemtafuta kwenye hospitali mbalimbali na maeneo mengine jijini Nairobi pasipo kufaulu.

Komu alieleza kwamba alipotizama kamera za uangalizi CCTV, alimuona akiingia na kutoka katika afisi za NLC baada ya kumfikisha kazini kabla yake kutoweka asijulikane aliko.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here