Mbunge wa Embakasi Mashariki Babu Owino amepata pigo baada ya mahakama kukataa kuondolewa kwa kesi ya jaribio la mauji dhidi yake.
Mlalamishi Felix Orinda kwa jina maarufu DJ Evolve alikuwa ameiandikia mahakama akiifahamisha kwamba alikuwa amemsamehe mbunge huyo na alitaka kuondoa kesi hiyo ili ajishughulishe na kuendelea kupona.
Hata hivyo. Hakimu mkuu Benard Ochoi amesema ombi hilo halikuafikia vigezo vinavyohitajika kuondoa kesi hiyo kwa sasa.
Hata hivyo hakimu huyo amesema hajafunga milango kwa ajili ya mazungumzo zaidi.
Ochoi amesema hawezi akakubali kuondolewa kwa kesi hiyo kwa sababu hajui Babu alimpa nini DJ Evolve.