Mtoto wake aliyekuwa gavana wa Kiambu Ferdinand Waititu ametozwa faini ya Sh30,000 au afungwe kifungo cha miezi mitatu jela baada ya kukutwa na hatia ya kuendesha gari akiwa mlevi.
Brian Waititu ameshtakiwa kwa kuendesha gari aina ya Toyota Probox katika barabara ya Muindi Mbingu akiwa mlevi kiasi cha kwamba alishindwa kulidhibiti.
Akikubali makosa hayo mbele ya hakimu mkuu wa mahakama ya Milimani Esther Kimilu, Brian aliomba asipewe adhabu kali kwa sababu hayo yalikuwa makosa ya kwanza.
Hakimu huyo alizingatia kilio chake na kumpa adhabu hiyo ya faini ya Sh30,000 au kifungo cha miezi mitatu jela.









