SERIKALI ya Kenya imepiga marufuku mikutano yote yenye hadhi ya kimataifa nchini angalau kwa muda wa mwezi mmoja kufuatia hofu ya virusi vya Corona.
Hatua hii ni miongini kwa juhudi zinazowekwa na serikali kuzia kuingia nchini kwa virusi hivyo ambavyo vilianzia China.
Haya yametangazwa na waziri wa afya Mutahi Kagwe ambaye pia amesema Kenya imeondoa marufuku ya muda kwa ndege moja kutoka Italia kuwaruhusu raia 800 wa taifa hilo waliokwama Malindi kurejea kwao.
Wakenya aidha wanashauriwa kujiepusha na kusafiri katika mataifa yaliyoathirika na virusi hivyo iwapo sio lazima wasafiri na kusisitiza kuwa ukaguzi wa lazima unafanyika katika viingilio vyake ili kuhakikisha kuwa homa hiyo haiingii nchini.









