Hali ya wasiwasi imegubika chuo kikuu cha Nairobi baada ya wanafunzi kuandamana kulalamikia muaji ya mwenzao.
Wanafunzi hao waliandamana Jumatatu usiku na kusababisha hasara ya mali isiyojulikana kupinga mauaji ya mwenzao wanayedai kuwa aliuawa na mmoja wa walinzi.
Marehemu Kyte Ochieng alifariki Jumamosi iliyopita akipokea matibabu katika hospitali kuu ya kitaifa ya Kenyatta (KNH).
Wanafunzi hao wanadai mwenzao alikamatwa na walinzi akiwa na wenzake wawili Jumatano wiki iliyopita walipokuwa njiani kurejea katika vyumba vyao vya malazi.