HALI TETE YA USALAMA MANDERA

0

Wakaazi wa Mandera Kaskazini mwa Kenya wanatoroka makwao wakihofia usalama wao kufuatia hali tete ya usalama inayosababishwa na mapigano baina ya vikosi vya usalama vya Somalia katika mpaka baina ya Kenya na Somalia.

Taharuki hiyo imesababishwa na vita kati ya majeshi ya Somalia na Jubaland katika eneo la Bula Hawa mapema wiki hii.

Wakiongozwa na gavana wa Mandera Ali Roba, viongozi hao wakizungumza jijini Nairobi wanasema wakaazi waliotoroka makwao wamesalia kuwa wakimbizi nyumbani kwao ilhali serikali haijafanya lolote kushughulikia hali hiyo.

Viongozi hao vile vile wametaka wanataka taifa jirani la Somalia kuachwa kushughulikia matatizo yake pasipo kuingiliwa ili kuwapa wakaazi usalama wao.

Kauli za viongozi hao zinajiri baada ya Ikulu ya rais Nairobi kuitaka Somalia kukoma kuingiza Kenya katika mgogoro wake wa uongozi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here