Bunge la kaunti ya Nairobi lapiga kura ya kumuondoa gavana Sonko

0

Gavana wa Nairobi Mike Mbuvi Sonko ametimuliwa baada ya wawakilishi wadi 88 kati ya 122 kupiga kura ya kuunga mkono hoja ya kumbandua.

Hoja hiyo iliwasilishwa bungeni na kiongozi wa walio wachache Michael Ogada akimtuhumu Sonko kwa matumizi mabaya ya afisi na ufisadi.

Bunge la kaunti ya Nairobi limepigia kura hoja hiyo licha ya kuwepo kwa agizo la mahakama linalozuia kujadiliwa kwake.

Yanajiri haya saa chache baada ya jaji James Rika kujiondoa kwenye kesi hiyo licha ya pingamizi kutoka kwa mawakili wa Sonko.

Sonko pamoja na wawakilishi wadi wanaomuunga mkono wamekuwa Kwale katika kile kilichoonekana kama juhudi za kujaribu kuzuia kuendelea kwa mjdala huo wa kumng’oa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here