Haki za kibinadamu zilikiukwa wakati wa corona yasema ripoti ya CRECO

0

Mwanamke mmoja alibakwa na wanaume sita katika eneo la Laini Saba, Kibra mnamo Agosti 30 mwaka huu.

Waliomtendea unyama huu ni watu waliokuwa wanamfahamu hiki kikiwa ni moja wapo wa visa vya ukiukaji wa haki za kibinadamu kilichorekodiwa kwenye ripoti iliyotolewa na mashirika ya kutetea haki za kibinadamu tangu Kenya ilipoanza kutekeleza masharti ya corona.

Katika eneo la Syokimau, kijakazi mmoja alipigwa hadi kungolewa meno na mwajiri wake alipoitisha mshahara wake baada ya kufanyakazi. Huko YMCA kaunti ya Nakuru, mwanamke mmoja aliuawa kwa kudungwa kisu na mwanamume mmoja baada ya kuzozana.

Hayo yakijiri

Mwalimu mmoja katika eneo la Changamwe, Mombasa naye alijinyonga nyumbani kwake baada ya kutofautiana na mkewe kutokana kila kilichotajwa kama hali ngumu ya kiuchumi iliyosababishwa na janga la corona.

Haya yote yako kwenye ripoti yenye kichwa ‘’Uchungu na Mateso wakati wa Janga’’ iliyotolewa na mashirika Ishirini na mbili ya kutetea haki chini ya mwavuli wa CRECO.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, visa vya watu kuzuiliwa kinyume cha sheria, polisi kutumia nguvu kupita kiasi na visa vya dhulma za kijinsia vimeongezeka.

Na huku idadi ya visa vya ugonjwa wa corona vikiendelea kuongezeka nchini, mashirika hayo yanahoji kwamba serikali imekosa kuwajibika vilivyo kukabiliana na janga hilo la kimataifa.

Utafiti huo ulifanywa katika kaunti za Nairobi, Kiambu, Mombasa, Kajiado, Busia, Nakuru, Kilifi, Migori na Uasin Gishu.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here