Kenya yaandikisha idadi kubwa ya watu waliopona corona

0

Kenya kwa mara ya kwanza imerekodi  idadi kubwa ya watu waliopona  ugonjwa wa corona baada ya watu 11,374  kupona katika muda wa saa Ishirini  na nne zilizopita.

Hii inafikisha idadi ya waliopona kufikia sasa kuwa 67,788.

Katibu mkuu katika wizara ya afya Dkt. Rashid Aman amedhibitisha visa 1,253 vya maambukizi mapya baada ya kupima sampuli 10,170 na kufikisha idadi ya visa hivyo kuwa 86,383.

Aidha watu wengine 16 wamefariki kutokana na ugonjwa huo na kufikisha idadi hiyo kuwa 1,500.

Nairobi imeandikisha visa 326, Mombasa 143, Kilifi 105, Kiambu 86, Muranga 67 na Meru 45.

Dkt. Aman amesema kwamba Kenya inaendelea kuwa na mangumzo na mataifa ambayo yameanza kutumia chanjo ya corona na huenda taifa likaanza kupokea chanjo hizo katika kipindi cha majuma machache yajayo.

Hayo yakijiri

Wamarekani wamekatazwa kusafiri kuja Kenya kwa sababu ya kuongezeka kwa maambukizi ya ugonjwa wa corona.

Marekani ambayo ni moja wapo ya mataifa yaliyoandikisha idadi kubwa ya visa vya ugonjwa huo pamoja na maafa imeiweka Kenya katika mataifa ya kiwango cha NNE sawa na Uganda, Tanzania na Burundi kumaanisha kuwa kiwango cha maambukizi kiko juu.

Kwenye tahadhari hiyo, Marekani imewakanya raia wake dhidi ya kusafiri Kenya kwa vyovyote vile na iwapo ni lazima waje basi wapimwe kati ya siku moja hadi tatu kabla ya kusafiri.

Takwimu nchini Marekani zinaonesha kuwa taifa hilo limeandikisha visa 14,000 vya ugonjwa huo maafa yakifikia 264,000.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here