Dhuluma dhidi ya wanawake wajawazito ni ukiukaji wa haki za kibinadamu ambao kwa miongo mingi imenyamaziwa.
Wakunga wanaripotiwa kuwa kwenye mstari wa mbele wa dhuluma hii; wakenya wengi wakiwahusisha na semi chafu dhidi ya akina mama wanaobanwa na uchungu wa uzazi.
Lakini je wajua kuwa dhuluma na maneno yasiyofaa dhidi ya akina mama hawa wenye mzigo nzito wa kuleta maisha huwa na athari ya kimwili kwao na kwa wanao. Anavyotuarifu Elvis Omondi shirika moja humu nchini limejitwika jukumu la kuhakikisha kuwa sharia inapitishwa kukomesha aina hii ya dhuluma.