Mbunge wa Kabuchai kaunti ya Bungoma James Lusweti Mukwe amefariki.
Kifo chake kimedhibitishwa na kiongozi wa chama chake cha FORD Kenya Moses Wetangula.
Mbunge huyo aliyekuwa anahudumu kwa muhula wa pili amefariki akipokea matibabu katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Mwili wake umepelekwa katika hifadhi ya Lee.
Rais Uhuru Kenyatta na naibu wake William Ruto wamewaongoza viongozi wengine kumuomboleza marehemu.
Rais amemtaja mwenda zake kama aliyekuwa mwenye kusema machache ila kazi yake ilikuwa inaonekana katika eneo bunge lake.
Wengine ni kinara wa chama cha Amani National Congress ANC Musalia Mudavadi, mwenzake wa ODM Raila Odinga, spika wa bunge la kitifa Justine Muturi ni miongoni mwa viongozi ambao wamemuomboleza marehemu.
Kifo chake kinawadia huku wakaazi wa Matungu wakiendelea kuomboleza kifo cha mbunge wao Justus Murunga.