Bunge kukata rufaa dhidi ya uamuzi wa kufutilia mbali miswada 23

0

Bunge la kitaifa litakata rufaa dhidi ya uamuzi wa mahakama kuu kufutilia mbali miswada 23 iliyopitishwa na bunge hilo kufuatia kesi iliyowasilishwa mahakamani na bunge la Senate.

Bunge hilo linasema uamuzi huo unakiuka katiba kwani ulikosa kuzingatia mamlaka ya bunge la kitaifa kikatiba.

Jopo la majaji watatu lilitaja hatua hiyo ya bunge la kitaifa kama isiyofaa na inayokiuka katiba.

Miswada hiyo inajumuishwa ule wa uhalifu wa kimtandao na ule ya shirika la vijana kwa taifa NYS.

Katika uamuzi wao, majaji hao waliamuru kwamba mabunge yote mawili yanafaa kushauriana kwenye miswada yoyote inayohusiana na kaunti.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here