Watalaamu wa afya wataka masharti makali ya corona kurejeshwa

0

Serikali imetakiwa kurejesha masharti makali ya kuzuia msambao wa virusi vya corona kufuatia kuongezeka kwa idadi ya visa hivyo katika siku za hivi karibuni.

Katika taarifa, muungano wa wataalamu wa afya nchini KMA unalaumu kulegezwa kwa masharti hayo kama sababu kuu ambayo imechangia kupanda kwa idadi ya visa hivyo nchini.

Kupitia rais wake Dkt. Andrew Onyino, muungano huo unataka mikutano ya kisiasa kupigwa marufuku kwa siku angalau kwa mwezi mmoja na kufungwa kwa kaunti zinazoshuhudia idadi kubwa ya virusi hivyo.

Muungano huo aidha umeelezea wasiwasi wake kuhusu idadi ya wahudumu wa afya wanaoendelea kuambukizwa virusi hivyo ambapo umesema walioambukizwa kufikia sasa ni 1,500 huku wengine wakiendelea kupigania maisha yao katika hospitali mbalimbali nchini.

Wahudumu hao wa afya aidha wanataka serikali kuwekeza zaidi katika sekta ya afya ili kuimarisha vita dhidi ya ugonjwa huo ikiwemo kuwaajiri matalaamu zaidi na pia kununua vifaa vya matibabu vitakavyopiga jeki vita dhidi ugonjwa huo.

Serikali aidha imetakiwa kukaza kamba katika kuwataka Wakenya kuvalia barakoa, kuepuka mikusanyiko na kudhibiti maeneo ya burudani ambayo yanakiuka masharti hayo ya usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here