Ruto asitisha mikutano yake ya kisiasa

0

Naibu rais William Ruto ametangaza kusitisha mikutano yake ya kisiasa kufuatia kuongezeka kwa idadi ya visa vya ugonjwa wa corona.

Kufuatia hatua hiyo, Ruto amehairisha mikutano yake katike eneo la Ukambani iliyokuwa imeratibiwa kuandaliwa wikendi hii.

Ruto alikuwa ameratibiwa kuendelea na mikutano yake ya kisiasa katika kaunti za Machakos, Makueni na Kitui.

Naibu rais ametangaza kuhairisha mikutano hiyo siku moja baada ya kukutana na wafanyibiashara kutoka kaunti hizo tatu katika afisi zake za Karen, Nairobi kupanga mikakati kabla ya ziara hizo.

Aidha, hatua ya Ruto inakuja siku moja kabla ya rais Uhuru Kenyatta kuongoza kikao kingine kujadili hali ya corona nchini ambapo kituo hiki kubaini kwamba pendekezo moja ni kupiga muarufuku mikutano ya kisiasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here