Baraza la LSK lapinga hatua ya Nelson Havi kumfukuza Mercy Wambua

0

Baraza kuu la chama cha Mawakili nchini (LSK) limepiga kura ya kupinga kufukuzwa kwa afisa mkuu mtendaji Mercy Wambua na rais Nelson Havi.

Katika taarifa hilo, baraza hilo baada ya kumpa Wambua nafasi ya kujitetea kufuatia tuhuma dhidi yake, wanachama tisa kati ya kumi na tatu walipiga kura kupinga uamuzi huo na kuafikia kuwa arejeshwe afisini mara moja.

Baraza hilo vile vile limemsuta Havi kwa kuwakosea heshima wanachama wake kupitia matamshi yake kwenye vyombo vya habari.

Na ili kumfundisha Havi namna ya kuongoza LSK, baraza hilo linashauri kuandaliwe kikao naye ili kumshauri.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here