Aisha Jumwa kulala seli

0

Mbunge wa Malindi Aisha Jumwa atazuiliwa hadi Alhamisi wiki hii wakati atajibu mashtaka ya mauaji yanayomkabili.

Jaji wa Mahakama kuu Margret Njoki Mwangi ameagiza Jumwa na mlinzi wake wa kibinafsi Geoffrey Okuto Otieno kuzuiliwa katika kituo cha polisi cha Port kutoa fursa kufanyiwa uchunguzi wa kiakili kabla ya kujibu mashtaka dhidi yao.

Wawili hao wanadaiwa kumpiga risasi Gumbao Jola mkesha wa uchaguzi mdogo wa Ganda kaunti ya Kilifi mwaka uliopita.

Tukiwa bado mahakamani…

Mahakama imeairisha kesi ya mauaji  ya wakili Willie Kimani, mteja wake na dereva wa teksi inayowakabili maafisa wanne wa polisi baada ya mmoja wao kupatikana na virusi vya corona

Hakimu Jessie Lessit amesema mmoja wa washukiwa hao Stephen Cheburet amepatikana na covid 19 na kwa mujibu wa kanuni za wizara ya afya, hafai kuwa mahakamani hadi atakapopata afueni.

Watatu hao waliuwawa Juni 23 2016 na kesi hiyo imertibiwa kusskilizwa Jumatatu wiki ijayo.

 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here