Wakenya wanatazamiwa kuanza kupokea kadi za Huduma Namba baada ya rais Uhuru Kenyatta na mkewe Margret Kenyatta kuwa wa kwanza kupokea kadi hizo.
Akizungumza katika hafla ya kuadhimisha siku ya Mashujaa kaunti ya Kisii Rais Kenyatta amesema kuwa Wakenya watapata kadi hizo baada ya bunge kumuidhinisha Immaculate Kassait kuwa kamishna wa data.
Akizungumza wakati wa kutoa kadi hizo, waziri wa usalama wa ndani Dkt. Fred Matiang’i amesema shughuli ya kutengeneza kadi hizo tayari imekamilika baada ya miaka miwili ya kusubiri na sasa kilichosalia ni kuanza kuzitoa rasmi kwa Wakenya.
Itakumbukwa kwamba wendani wa naibu rais William Ruto wakiongozwa na wabunge Aisha Jumwa wa Malindi na mwenzake wa Kikuyu Kimani Ichungwa wamenukuliwa wakidai kwamba Huduma Namba ni njama ya kumuibia Ruto kura wakati wa uchaguzi mkuu wa 2020.
Wakenya wengine kumi walipata kadi hizo huku rais Kenyatta akisema kadi hiyo itawasaidia Wakenya kupata huduma za serikali kwa urahisi.