Baba anayedaiwa kumuua mwanawe wa miaka minane kwa kumchoma na maji moto katika eneo la Sigor kaunti ya Pokot Magharibi ameshikwa na makachero wa DCI.
Mshukiwa huyo Madangure Chelonges anadaiwa kumkabili mwanawe kinyama baada ya kuzozana tarehe kumi na saba mwezi huu wa Januari.
Mtoto huyo baadaye alifariki akiendelea kupokea matibabu hospitalini kutokana na majeraha aliyoyapata.
Baba huyo anaendelea kuzuiliwa akisubiri kufikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa uchunguzi.