Mahakama yamtia breki kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu

0

Hatma ya kaimu jaji mkuu Philomena Mwilu kuendelea kushikilia wadhifa wa jaji mkuu inasalia kwenye mizani baada ya mahakama kutoa agizo linalomzuia kufanya hivyo.

Jaji wa mahakama ya Meru Patrick Otieno pia imetoa agizo linalomzuia kuendelea kuhudumu kama jaji wa mahakama ya upeo na mwanachama wa tume ya huduma za mahakama (JSC) hadi kesi dhidi yake itakaposikilizwa na kuamuliwa.

Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani na wakili Isaiah Mbiti anayemtuhumu Mwilu kwa matumizi mabaya ya afisi.

Uamuzi huu wa kumzuia Mwilu kuhudumu katika tume ya JSC utamzuia kushiriki kwenye mchakato wa kumtafuta mrithi wa David Maraga kama jaji mkuu maombi yakitazamiwa kutumwa kufikia Februari 10.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here